Change Agents The Podcast

(Swahili) A Moment of Pause: Navigating Misinformation in Immigrant Communities

Reparations Media Season 6 Episode 10

Use Left/Right to seek, Home/End to jump to start or end. Hold shift to jump forward or backward.

0:00 | 17:51

Katika sehemu hii, Emma Yaaka, mkimbizi kutoka Uganda na mtetezi wa jamii, anaeleza jinsi habari za uongo zinavyoenea kupitia mitandao ya wakimbizi na wahamiaji na madhara halisi yanayoweza kutokea. Kuanzia makundi ya WhatsApp hadi TikTok na YouTube, hofu inaweza kuenea haraka, ikichochea maamuzi kuhusu afya, usalama, na hata kuhama. Emma anafanya kazi na jamii yake kusubiri, kuhakiki, na kupata habari katika mazingira ambapo uaminifu ni mdogo na hatari ni kubwa. Wataalamu Dkt. Zach McDowell wa UIC na Dkt. Michael Spikes wa NU-Medill wanaelezea kwa nini kutofautisha kati ya habari zisizo sahihi (misinformation) na habari za uongo za makusudi (disinformation) ni muhimu — na kwa nini mahusiano yanayoaminika yanaweza kuleta tofauti kubwa. 

Kipindi hiki kimetayarishwa na Grace Asiegbu, sehemu hii inachunguza jinsi habari za kidijitali, hofu, na jamii zinavyokutana katika maisha ya wakimbizi. Kipindi hiki kimetayarishwa na Grace Asiegbu @epitome_of_grace kwa ajili ya Reparations Media NFP | Kwa ushirikiano na Emma Yaaka na U.S. Refugee Integration Organization.

### 

In this episode, Emma Yaaka, a Ugandan refugee and community advocate, shares how misinformation spreads through refugee and migrant networks and the real consequences it can have. From WhatsApp groups to TikTok and YouTube, fear can travel fast, shaping decisions about health, safety, and even relocation. Emma works with his community to pause, verify, and navigate information in an environment where trust is fragile, and stakes are high. Experts Dr. Zach McDowell of UIC and Dr. Michael Spikes of NU-Medill explain why distinguishing misinformation from disinformation matters — and why trusted connections can make all the difference. 

Produced by Grace Asiegbu, this episode explores how digital information, fear, and community intersect in the lives of refugees. Produced by Grace Asiegbu @epitome_of_grace for Reparations Media NFP | In collaboration with Emma Yaaka and U.S. Refugee Integration Organization.





Support the show


Grace Asiegbu : [00:00:01] Emma Yaaka anafanya kazi kwa karibu na jamii za wakimbizi na wahamiaji na anaona jinsi taarifa zinavyoweza kushika kasi kwa haraka.

Emma Yaaka : [00:00:14] Uhofu mwingi katika jamii zetu za wakimbizi na wahamiaji inaanza na taarifa za mtandaoni. Mitandao tunayopenda sana kutumia ni YouTube, TikTok na WhatsApp. Mimi niko kwenye makundi mingi ya WhatsApp karibu hamsini. Kikundi moja za makundi hizi kiko na watu mia mbili hamsini na taarifa husambaa haraka sana kwenye makundi haya.

Grace Asiegbu : [00:00:46] Akiwa mkimbizi kutoka Uganda yeye mwenyewe, Emma anajua jinsi taarifa zinavyoweza kusambaa kwa haraka mtandaoni na ameona jinsi taarifa zisizo sahihi zinavyosambaa kwa kasi ile ile zikichochea hofu katika nyakati ambazo tayari zina mvutano na sintofahamu. Hadhi zana za kidijitali zinavyozidi kuwa za kisasa kuanzia video zilizobadilishwa hadi maudhui yanayoendeshwa na algoritimu yaliyoundwa kuchochea hisia. Kutenganisha kilichohalisi na kisichohalisi kumekuwa kugumu zaidi na athari zake ni kubwa kuliko hapo awali. Kwa wakimbizi na wahamiaji, taarifa potofu zinaweza kudharimu afya yao, riziki yao au hata hadhi yao ya kisheria. Mimi ni Grace Asiebu na hii ni podkasti ya Change Agents. Moja ya vyanzo vikubwa vya hofu kwa wakimbizi na wahamiaji imekuwa tishio linaloendelea la maafisa wa serikali kuu katika jiji. Wakati wa utawala wa Donald Trump katika msimu wa vuli wa mwaka wa elfu mbili na ishirini na nne, kulikuwa na operesheni iliyotekelezwa mjini Chicago ambayo maafisa waliita Operation Midway Blitz. Kulishuhudiwa maafisa wa ICE wakifanya msako katika eneo la Chicagoland wakiaacha hali ya vurugu na taharuki nyuma yao.

Emma Yaaka : [00:02:35] Watu wanasema ICE inafukuza kila mtu. Je, hiyo ni kweli? Ni kila mtu anafukuzwa.

Grace Asiegbu : [00:02:45] Kwa sababu taarifa husambaa kwa kasi sana, hasa kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook na WhatsApp, hata pale ambapo hakuna nia mbaya, madhara yanaweza kuwa ya kudumu.

Emma Yaaka : [00:03:03] Mteja wangu alikuwa mgonjwa na alifanyiwa upasuaji Nilikuwa hospitali pamoja naye. Muongoozi mmoja kutoka Afrika mwenye anafanya hiyo hospitali alimuambia usikae hospitali muda mrefu sana. ICE inaweza kukukamata au ikurudishe kwenu. Kwa sababu ya uhofu, alilazimisha kuruhusiwa kuenda nyumbani mapema. Hii limfanya achukue muda mrefu kupona kwa sababu hakupata huduma mzuri nyumbani juu alikuwa anaishia peke.

Grace Asiegbu : [00:03:39] Emma anasema mfano huu ni moja tu kati ya mingine mingi kama hii ambayo ameiona au kusikia. Huku wakimbizi wakijaribu kupitia safari ya kuchanganya ya kuanza maisha mapya katika kipindi cha mvutano wa kisiasa unaozidi kuongezeka.

Emma Yaaka : [00:04:04] Wahamiaji wawili na wakimbizi wawili wenye nilikuwa nasaidia sana waliamua kuhama jimbo hii waondoke waende jimbo lingine. Mi hivi mwenyewe nilisaidia mmoja kusafiri usiku kwa basi. Wanaona hapa hakuna salama tena. Ingawa hawajaona wenyewe, ni taarifa tu kutoka mitandao ya kijamii.

Grace Asiegbu : [00:04:35] Hadithi kama hizi zinaonyesha jinsi taarifa zisizo sahihi zinavyoweza kuathiri maamuzi kwa wakati halisi. Kwa wakimbizi wengi, taarifa hutoka katika maeneo yanayofahamika, vyombo vya habari vya nchi zao za asili, wahamiaji wengine na watu wanaozungumza lugha yao. Iwe ni sahihi au laa, vyanzo hivi vina uzito kwa sababu vinaonekana kufahamika na vinaaminika. Ndiyo maana ni muhimu kutofautisha aina mbili kuu za taarifa zisizo sahihi: taarifa potofu na taarifa za kupotosha kwa makusudi. Daktari Zach McDowell, profesa wa mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Illinois Chicago, anaeleza kuwa ingawa taarifa zisizo sahihi zinaweza kuwa na madhara, hazijauundwa kwa namna au kwa nia sawa.

Zach McDowell : [00:05:48] Habari ambayo si ya ukweli ama ni sawa haiko kwa kutumika hapa. Wacha niseme kwa uzuri lakini ni vibaya kwa kupeana habari ambayo haihitajiki, si ya ukweli

Zach McDowell : [00:06:08] Ama kudanganya ama kwa kutoa habari yoyote.

Grace Asiegbu : [00:06:12] Kulingana na McDowell, tofauti hiyo ni ya msingi sana. Lakini hata taarifa potofu ambazo mara nyingi husambazwa kwa nia njema, zinaweza kusababisha madhara halisi, kama ilivyokuwa kwa mteja wa Emma hospitalini. Muuguzi hakuwa akijaribu kumpotosha mtu yeyote, lakini alikuwa mtu mwenye mamlaka akizungumza na mtu ambaye hali yake ya uhamiaji tayari ilifanya kila uamuzi uonekane kuwa na hatari kubwa. Muuguzi, kama mteja huyo na wengine wengi, alikuwa akifanya kazi ndani ya mazingira hayo hayo ya hofu.

Zach McDowell : [00:07:03] Hata wakimaliza kuona kwamba wametoa watu, um, hapa warudisha kwao ni vibaya. Lakini watu wengi wanamaliza hakuna kitu ambaye wamefanya. Wengine, um, wanashikwa, wengine wameongezeka kwa kuokopa sana, sana, sana. Kama umeokopa haujui kitu ambayo inafuatilia. Ukiongeza mambo ama shida ambayo wanapitia hapa. Watu wengi hawawezi kukubali ama kupata hiyo habari kwa ukweli. Wengine wako hawako na watu wao hapa. Hii inamfanya watu kuwa vigumu sana. Hiyo ni shida kubwa saa hii. Kukubali mtu ama kuona kwamba unakubali kitu mtu ama ukweli.

Grace Asiegbu : [00:08:04] Ikiwa kila mtu anapata taarifa mtandaoni, kwanini uaminifu unapotea? Emma anasema sehemu ya jibu ni tamaa ya kusambaa haraka mtandaoni.

Emma Yaaka : [00:08:19] Waundaji wa maudhui, hata mimi mwenyewe, tunaangalia vitu vinavitrend. Kabla ukweli ijafika, taarifa tayari zimeumiza watu. Amani inachukua muda mrefu kujengwa, lakini inaweza kuvunjika haraka sana kwa sababu ya taarifa.

Grace Asiegbu : [00:08:46] Anachokielezea Emma kinazidi mitandao ya kijamii ni kuvunjika kwa mfumo wa vyombo vya habari. Ili kuelewa kwanini, nilizungumza na Daktari Michael Spikes, mtaalamu wa taarifa potofu katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Medill, Northwestern University na mkurugenzi wa programu yake ya Teach for Chicago Journalism. Anasema mipaka kati ya habari zilizoripotiwa, maoni ya uchambuzi na maoni ya kawaida imefifia kabisa. Huku watu wakitumia muda mwingi zaidi mtandaoni na vyombo vya habari vya kuripoti vikizidi kutoweka.

Michael Spikes : [00:09:39] Kutokana na muda mwingi ambao watu hutumia kwenye majukwaa haya na pia muda ambao imewachukua watu kukuza tabia hizi za kuamini aina hii ya taarifa, ningesema kwamba ule mstari umefutika kabisa.

Grace Asiegbu : [00:09:56] Wakati hofu inapochukua nafasi ya uaminifu, akili hutafuta uhakika, si usahihi.

Michael Spikes : [00:10:06] Kwa kweli, jambo kuu ni hili. Watu wanapokuwa na hofu au wanapofanywa waogope kitu fulani, uwezo wao wa kuwa na mashaka au uwezo wao wa kudhibitisha, kuchambua au kutathmini taarifa huanza kutofika, kwa sababu tunaingia katika hali ya kupambana au kukimbia. Kwa hiyo, tunaelekea zaidi kwenye taarifa ambazo zinaonekana kuwa na uhakika zaidi. Na katika baadhi ya matukio, tutatumia dalili fulani kama vile nguvu au msisitizo wa taarifa hiyo kama ishara ya kutuaminisha kwamba lazima iwe sahihi zaidi bila sisi kuwa na uwezo wa kugundua au kutathmini kama taarifa hiyo inaungwa mkono na ushahidi au kama kuna kitu kinachodhibitisha ukweli wake mbele yetu.

Grace Asiegbu : [00:11:08] Hofu haiji peke yake. Na hapa ndipo kundi la WhatsApp la watu mia mbili na hamsini ambalo Emma Yumo linaweza kuongeza hali ya taharuki. Katika kundi ambalo watu wanashiriki uzoefu wao mgumu wa maisha na wanajaribu kuishi katika mazingira yanayohisi kama ufuatiliaji wa karibu, kitu kidogo tu kinaweza kukuzwa na kuwa kikubwa. Wajumbe wanaoaminika kama Emma hufanya juhudi zao kuelimisha na kudhibitisha taarifa. Lakini katika mazingira ya vyombo vya habari yanayothamini wingi na kasi kuliko usahihi, taarifa potofu kuwa hatari zaidi, hasa kwa wakimbizi na wahamiaji.

Michael Spikes : [00:12:11] Na ningesema hata zaidi kwamba ujio wa simu janja na upatikanaji wa intaneti uliopo kila mahali utatufanya kuwa kama tuko chini ya ushawishi fulani wa kuweza kupata taarifa haraka. Na tunachanganya kasi ya kupata taarifa hiyo na kiwango cha kuaminika kwa taarifa yenyewe.

Grace Asiegbu : [00:12:35] Kwa Emma, sehemu ya kazi yake ni kushughulikia hali hii ya sintofahamu kutoka kwa wateja wake na jamii yake.

Emma Yaaka : [00:12:48] Kadri wanavyopokea taarifa, wanazituma kwangu kwa sababu wananiamini. Wanasema, tazama hii nini kinaendelea. Tuko salama? Tutakuwa sawa hapa?

Grace Asiegbu : [00:13:04] Anapokumbana na maswali haya, jukumu la Emma sikua na majibu yote. Ni kuwasaidia wakimbizi wenzake kusimama kidogo kwa muda wa kutosha ili wao wenyewe waweze kuuliza maswali zaidi. Kusimama huko ni sehemu muhimu ya uelewa wa vyombo vya habari.

Michael Spikes : [00:13:32] Elimu ya uelewa wa vyombo vya habari unaweza kuita kwa majina mengine kama ujuzi wa kidigitali. Vitu hivi vyote vinahusu kujifunza jinsi ya kuvunja au kuchuja ishara hizo. Unajifunza jinsi ya kuzitambua na kujenga kiwango cha juu cha mashaka yenye afya juu ya madai unayoweza kusikia. Hata kama yanatoka kwa watu unaowajua au unaowafahamu. Lakini pia unatambua kwamba wakati mwingine unapaswa kupokea wanachosema kwa tahadhari. Kwa sababu wenda hawana utaalamu wa kutosha kuhusu kile wanachozungumzia. 

Grace Asiegbu : [00:14:18] Wataalamu wote wawili wanakubaliana kwamba hata kwa mafunzo yote duniani, athari kubwa zaidi kutoka kwa watu wanaotuzunguka. Marafiki na wanajamii tunawamini kutusaidia kuelewa na kuchuja taarifa ambazo hatuwezi kuzibiditisha kila wakati sisi wenyewe. Huyu hapa ni Zach McDowell kutoka Chuo Kikuu cha Illinois, Chicago.

Zach McDowell : [00:14:54] Unaweza kuitwa kwa sherekeo na pati ama kitu yoyote na mtu yeyote. Marafiki zako wakakuita ukuje lakini hauwezi kuwa na ukweli kwamba huyo mtu ni sawa. So kwa kuenda hapo si rahisi sana sana kwa sababu hauko na mtu ambaye unaweza ona. So inamanisha kwamba kwa kushika marafiki inakuwa shida sana. Haujui mtu gani ndio ako sawa. Lakini hii ndio kitu ambayo tunatakikana  kuona kwamba tunafanya hii kazi kwa kubwa.

Grace Asiegbu : [00:15:34] Hata ndani ya mitandao ya kuaminika, kutambua dalili za taarifa potofu huwasaidia watu kufanya maamuzi bora na salama.

Zach McDowell : [00:15:48] Inaweza kuangalia kwamba ni sawa kitu ambayo inalingana na hamu ambayo uko nayo lakini kwa kufanya kitu ingine ambayo imewekwa kwa hiyo haiwezi badilika.

Grace Asiegbu : [00:16:04] Wazo hilo kusimama kidogo na kuhoji mambo yanayoonekana kufaa kupita kiasi sio la kinadharia ndio kazi ambayo Emma hufanya kila siku. Kila ujumbe wa WhatsApp anaochunguza unasaidia jamii yake kusimama kabla hofu haijawafanyia uamuzi. Ujumbe moja wa moja kwa moja kwa wakati mmoja.

Close: [00:16:49] Thank you for joining Change Agents, the podcast series looking at grassroots actions and solutions through stories told from the inside out. Change Agents is produced by Reparations Media. The music is composed by Sarah Abdullah. Funding support is provided by the Chicago Community Foundation, the Chicago Community Trust, the Field Foundation, the Wayfarer Foundation, and the Lumpkin Family Foundation. Subscribe to this podcast on Apple Podcasts, Spotify, Stitcher, and wherever you find podcasts. And follow Change Agents on Facebook, Instagram, and our website, changeagentsthepodcast.com.