MAELEZO PODCASTS
Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.
MAELEZO PODCASTS
Latest Episodes
Tahadhari ya Mvua za El Niño Kuanzia Oktoba, 2026
Kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya uwepo wa mvua kubwa za El Nino, kupitia Maelezo Podcast ili kupata ufafanuzi tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a ambaye anaeleza k...
Aina Tatu za Saratani Zinazoathiri Maisha ya Wengi Nchini.
Katika kujenga uelewa kuhusu ugonjwa wa saratani, kupitia Maelezo Podcast tumemualika Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dkt. Chrispin Kahesa, tumezungumza kuhusu saratani na namna inavyoathi...
Changamoto ya Afya ya Akili, ni Akina Nani Waathirika Zaidi?
Kupitia Maelezo Podcast tunajadili kuhusu afya ya akili kwa kumualika Daktari Veronica Lyimo, Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili kutoka Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania, ambaye anatupitisha kwenye visababishi vya changamoto ya afya ya akili, ...
Kwanini ni marufuku kutunza kwa kutupa fedha chini?
Mazungumzo na Bw. Atufigwege Mwakabalile, Afisa Mwandamizi wa Benki kutoka Benki Kuu Tanzania (BOT) kuhusu sheria ya fedha nchini na marufuku iliyotilewa ya kutotunza fedha kwa kutupa chini.
Sheria ya Kuasili Mtoto (Child Adoption) Tanzania
Kupitia MAELEZO PODCASTS leo tunazungumza na Bi. Ludovicka Samare, Afisa Ustawi Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, anatupitisha kwenye utaratibu na Sheria ya kuasili mtoto (Child Adoption), nchini Tanzania