MAELEZO PODCASTS
Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.
Episodes
12 episodes
Siri ya Tarehe 7 Julai na Historia ya Tanzania Iliyowafanya UNESCO kuichagua kuwa Siku ya Kiswahili Duniani
Mazungumzo na Profesa Rehema Erasto., Mhadhiri wa Kiswahili kutoka Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma kuhusu historia ya siku ya Kiswahili Duniani, nafasi ya lugha za kijamii (makabila), makosa kwenye lugha ya kiswahili na namna ya kusah...
Kwanini Kongamano la Kiswahili Ufaransa na si kwingine? Majibu ya Msemaji Mkuu wa Serikali
Gerson Msigwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; na Msemaji Mkuu wa Serikali akitoa majibu ya ni kwanini Kongamano la Kiswahili la Pili la Kimataifa limefanyika nchini Ufaransa na si kwingineko.Pia tumezungumz...
Kuelekea Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa, Paris - Ufaransa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inatarajia kufanya Kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili kati ya Julai 4 - 7, 2026, jijini Paris, Ufaransa...
Fursa, Ushirikiano kati ya Algeria na Tanzania: Balozi Matinyi
Mheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Algier...
Balozi Kombo Aeleza Umuhimu wa Ziara ya Rais Samia katika Kuimarisha Mahusiano ya Tanzania na Urusi
Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 7 Juni, 2026.
Miaka 10 ya BMH: Jinsi Hospitali ya Benjamin Mkapa Ilivyobadilisha Huduma za Kibingwa Tanzania
Hospitali ya Benjamin Mkapa ni hospitali ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma, iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa ambazo kwa sasa zipo 20 na ubingwa bobezi zipo 17 kwa wananchi wa Tanzania na nchi jirani.
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 (Mei 4, 2026)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Mei 4, 2026, bungeni, jijini Dodoma.
Hotuba ya Mhe. Rais Samia na Mhe. Rais, Paul Kagame, Mei 03, 2026
Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, amefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania, akizungumza na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...
Hotuba ya Rais, Dkt. Samia Kwenye Kongamano la Biashara Baina ya Tanzania na Kenya, Mei 4, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Kenya (Tanzania & Kenya Business Forum 2026), tarehe 04 Mei, 2026, JNICC, jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hi...
Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando
Pata ufahamu sahihi kuhusu chanzo, dalili, matibabu pamoja na kinga ya ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell) na Dkt. Catherine Mhando wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.
Elimu kwa umma kuhusu zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI (2022)
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala. Halikadhalik...